Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. Charles John Mwijage (MP)

Wasifu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji awasilisha Hotuba ya Bajeti kwa mwaka 2017/2018


Imewekwa: 17th May, 2017

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage awasilisha Hotuba ya mapato na matumizi kwaka 2016/2017 na utekelezaji wa fedha za bajeti iliyopewa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Katika hotuba yake mhe. Mwijage ameeleza mikakati ya wizara katika kufikia adhima ya serikali ya Viwanda ifikapo mwaka 2025. Wizara imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini kupitia Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI). Pia waziri ameeleza maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa na Serikali chini ya mpango wa SEZ katika maeneo ya Kigoma (KISEZ) hekta 3,000; Bunda (Bunda SEZ) hekta 1,360; Ruvuma-SEZ hekta 2,033; Manyoni-SEZ hekta 1,909, kwa mwaka 2016/2017, eneo lenye ukubwa wa hekta 63,000 lililopo Mkulazi-Morogoro limekabidhiwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kwa ajili ya kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari chini ya Mkulazi Holdings Co. Ltd iliyoundwa kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza mradi huo.

Hatimiliki © wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji 2018. Haki zote zimehifadhiwa.