Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. George Joseph Kakunda (Mb)

Wasifu

ziara ya Naibu Waziri Mhe. Injinia Stella Manyanya Mkoani, Dodoma.


Imewekwa: 13th October, 2017

Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya afanya ziara yake ya kwanza ya kikazi akiwa Wizara ya Viwanda kwa kutembelea kongano la ngozi na bidhaa za ngozi katika eneo la zuzu Mkoani Dodoma. Aidha Mhe. Waziri amewaagiza watendaji wa wizara kufanya juhudi za haraka za uendelezwaji wa eneo hilo kwa hakuna sababu ya kuchelewa ambapo mhe. Naibu waziri ametoa muda wa miaka miwili hilo eneo liwe limeanza kuwekewa miundombinu na huduma nyingine. Pia mhe. Waziri ametembelea eneo la SIDO lililotengwa kwa ajili ya kongano la alizeti lenye ukubwa wa ekali 11 ambapo gharama ya mradi ni bilioni 4 pia amewaagiza watendaji kufanya juhudi za haraka kuharakisha mchakato wa uendelezwaji wa eneo hilo, Mhe. Naibu waziri alihitimisha ziara yake kwa kutembelea ofisi za SIDO na kutembelea ajasiliamali walioko chini ya SIDO na kujionea shughuli za ujasiriamali zinazofanywa katika eneo hilo. Mhe. Naibu waziri ataendelea na ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara kuanzia wiki ijayo na kujionea utendaji wa kila taasisi.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2019. Haki zote zimehifadhiwa.