Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Hon. Charles John Mwijage (MP)

Wasifu

Tanzania yatia saini Makubaliano ya uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA)


Imewekwa: 23rd March, 2018

Tanzania yatia saini Makubaliano ya uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Tanzania ni miongoni mwa nchi 44 zilizotia saini makubaliano ya uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (Africa Continental Free Trade Area –AfCFTA) katika mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Kigali tarehe 21 Machi, 2018. Makubaliano haya yanahusisha ushirikiano wa biashara ya bidhaa, biashara ya huduma, uwekezaji, masuala ya ushindani na haki miliki. Kusainiwa kwa makubaliano haya kunatoa fursa ya kiuchumi kwa kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika. Utekelezaji wa makubaliano haya utawezesha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kufikia malengo ya Ajenda 2063 na hatimae kuwa na Jumuiya ya Uchumi ya Afrika. Makubaliano haya yanatoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika, ikiwemo Tanzania, kwa kuleta pamoja soko la nchi wanachama wa Umoja wa Afrika 55 zenye takriban watu bilioni 1.2 na fursa katika uchumi unaokua kwa kasi. Makubaliano haya yanatarajiwa kuongeza mchango wa Afrika kwenye soko la dunia huku sekta za kilimo, chakula na huduma zikiwa na nafasi kubwa zaidi ya ukuaji huo.

Hatimiliki © wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji 2018. Haki zote zimehifadhiwa.