Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
Kongamano la Kaizen Barani Afrika  2021 (AKAC2021)   Agosti 24 - 26, 2021, Dar es Salaam

Kongamano la Kaizen Barani Afrika 2021 (AKAC2021) Agosti 24 - 26, 2021, Dar es Salaam

2021-08-24 To 2021-08-26 | Venue | Hyatt Regency Dar es Salaam, Tanzania and online/webinar

Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi za Afrika zilizoko katika mstari wa mbele wa matumizi ya falsafa ya KAIZEN inatarajia kuwa mwenyeji wa Kongamano  la Kaizen Barani Afrika la mwaka 2021 (AKAC2021), ambalo litatumika kushirikisha wadau kuhusu mafanikio na kubadilishana  uzoefu uliokwishapatikana; habari na kuchochea ushirikiano wa kikanda wa kukuza viwanda kupitia harakati za kueneza falsafa ya Kaizen / QPI Barani Afrika. Kongamano hilo litafanyika tarehe Agosti, 24 - 26, 2021 katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Tanzania na kwa njia ya mtandao.

Kauli Mbiu

Fursa za Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda na Biashara Barani Afrika: Ujumbe unaosisitizwa hapa ni uzingatiwaji wa matumizi ya Falsafa ya KAIZEN (Uongezaji Ubora & tija - QPI) na Teknolojia za Dijitali, katika Uanzishaji na Uendelezaji wa Viwanda vidogo na Biashara Ndogo na shughuli za kiuchumi majumbani ili kukuza uchumi wa ndani Barani Afrika. Kaulimbiu hiyo inatafsiriwa kwa lugha ya kiingereza yaani: `Opportunities to Accelerate Industrialization and Trade in Africa: Streamlining KAIZEN (Quality & Productivity Improvement - QPI) with Digital Technologies, Start-ups, SMEs Development and Home-Grown Economic Activities in Africa’.

Ratiba Wadhamini Watoa Mada Soma zaidi