Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. Prof Kitila Mkumbo (MP)

Wasifu

Katibu Mkuu aongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) ya Uwezeshaji Biashara.


Imewekwa: 03rd September, 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki S. Shemdoe Leo tarehe 3 Septemba, 2020 ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) ya Uwezeshaji Biashara katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini Dodoma. Lengo la kikao hiki lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa maelekezo ya mkutano wa kwanza wa kamati hiyo uliofanyika tarehe 13 Februari 2020. Masuala yaliyojadiliwa na kuidhinishwa ni pamoja na hadidu za rejea (ToR) za kamati ya kitaifa ya uwezeshaji biashara, Maeneo ya kundi A, B na C ya mkataba wa uwezeshaji biashara wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO TFA) ambayo yatawasilishwa sekretarieti ya WTO kabla ya tarehe 22 Septemba, 2020. Utekelezaji wa masuala mengine ya biashara nje ya mkataba wa uwezeshaji biashara, utekelezaji wa mpango mwelekeo (Roadmap) wa miaka mitano (2020/21 - 2024/2025) na mpango kazi (Action Plan) ya mwaka 2020/2021. Aidha, Kamati imetoa maelekezo ya maboresho ya Mfumo wa taarifa za ufanyaji biashara (National Trade Information Module) kabla ya kufanyiwa uzinduzi rasmi.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2021. Haki zote zimehifadhiwa.