Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. Prof Kitila Mkumbo (MP)

Wasifu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara akabidhiwa Ofisi Rasmi


Imewekwa: 14th April, 2021

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James amekabidhiwa ofisi rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Riziki Shemdoe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI leo katika ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizopo Mtumba jijini Dodoma. Makatibu Wakuu hao waliahidi kuendelea kushirikiana katika kazi mbalimbali hasa katika kuboresha muundo wa Maafisa Biashara wa Halmashauri kwa kuanzisha wa Kitengo cha Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili kurahisisha utendaji kazi wa wizara hizo kukuza biashara na kuendeleza viwanda vikubwa na vidogo vidogo vilivyopo katika halmashauri hizo. Akiwashukuru wafanyakazi wote wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kufanya naye kazi vizuri kwa ushirikiano na Amani, Katibu Mkuu TAMISENI alitoa angalizo kwa Wizara kuendelea kusimamia na upatikanaji wa Sukari, Mafuta ya Kula, Mfumuko wa bei wa vyakula hasa katika mfungo wa mwezi ramadhani, na masoko kwa ajili ya mazao ndani na nje ya nchi.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2021. Haki zote zimehifadhiwa.