Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji awasilisha Vipaumbele vya sekta ya Viwanda na Biashara katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2022/2023.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.  Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) ameliomba Bunge kuidhinishia Sh.Bilioni 99.1 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na taasisi zake. 

Aidha, Dkt. Kijaji ameainisha vipaumbele mahsusi 15 vya Mwaka wa fedha 2022/23, ikiwamo kuimarisha mifumo ya kushughulikia changamoto za uwekezaji na kutafuta fursa za masoko na kuwaunganisha na wajasiriamali wa ndani. Akisoma bungeni Mei 6, 2022  makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2022/23, Dkt.Kijaji amesema kwa kipindi hicho imepanga kuendelea kuratibu programu za uhamasishaji wa uwekezaji ndani na nje ya nchi. 

Akitaja vipaumbele vya Wizara, Dkt. kijaji amesema Wizara imepanga kuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi na kuratibu ufanikishaji wa uwekezaji ikiwemo kuongeza ufanisi wa miradi ya uwekezaji kupitia 

Vipaombele vingine alivyovitaja ni pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji yenye manufaa mapana kwa Taifa na kuboresha mazingira wezeshi ya kuendeleza viwanda na biashara kwa kupitia na kutunga sheria, sera na mikakati ya kuvutia uwekezaji. 

Pia ametaja kuimarisha na kuhamasisha uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zitakazouzwa nje (EPZ). 

Vipaumbele vingine ni kuimarisha taasisi za utafiti na kufanya tafiti kwa ajili ya maendeleo ya viwanda, kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini na bidhaa zinazotumiwa kwa wingi nchini kama vile nguo, mafuta na sukari na  kuendeleza viwanda vya usindikaji vinavyozalisha bidhaa za petroli (Petro-gas), kemikali, uzalishaji wa dawa za binadamu na vifaa vya ujenzi. 

“Kuratibu programu za kuimarisha Mifumo ya Udhibiti wa Biashara inayolenga katika kupunguza gharama za uwekezaji na kufanya biashara; Kuimarisha mifumo ya uratibu na usimamizi wa masuala ya uwekezaji kitaifa;Kushughulikia masuala ya ubora na viwango nchini,”amesema Dkt Kijaji.