Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Naibu Katibu Mkuu Dkt. Hashil Twalib Abdallah aongoza kikao na Taasisi ya Gs1 Tanzania


Naibu Katibu Mkuu Dkt. Hashil Twalib Abdallah aongoza kikao na Taasisi ya Gs1 Tanzania wanaohusika na kutoa misimbo milia (Barcodes) katika bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini, kikao kimefanyika katika ofisi za wizara Mtumba.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la Gs1 kutoa maelezo kwa kina kuhusu shughuli zao wanazozifanya kwenye masuala ya kutoa huduma za barcodes kwa wajasiriamali na pia kumuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kuwa mgeni rasmi tarehe 28 Agosti, 2021 kwenye kilele cha kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi hii.

kikao hiki kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange, Mjumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania Bi. Joyce Mapunjo na Dkt. Purificator A. Kiwango Mtafiti na Mkuu wa Kitengo cha Chakula kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).