Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Mipakani (OSBP) Kasumulu Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo tarehe 07 Agosti, 2022 ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Mipakani (OSBP) Kasumulu Wilayani Kyela Mkoani Mbeya mpakani mwa Tanzania na Malawi.
 
Ujenzi wa Kituo hiki ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kurahisisha ufanyaji Biashara baina ya nchi zinazopakana na Tanzania.
 
Hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.