Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa  Kuboresha Mazingira ya  Biashara nchini (Blueprint) ili  kuvutia uwekezaji na  kuwezesha ufanyaji biashara


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa  Kuboresha Mazingira ya  Biashara nchini (Blueprint) ili  kuvutia uwekezaji na  kuwezesha ufanyaji biashara wenye tija  utaokuza uchumi wa  taifa kwa ujumla. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo  wakati  alipokutana na kufanya mazungumzo na 
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia Ukuzaji wa Uchumi na Taasisi kutoka Benki ya Dunia (WB), Dr.Asad Alam na ujumbe wake kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma Septemba 29, 2022. 

Akiwa ameambata na Viongozi wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara akiwemo  Naibu Katibu Mkuu  Dkt. Hashil Abdallah,  Dkt. Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha na kuendeleza programu mbalimbali za kuwawezesha wajasikiamaki wadogo na wa kati kuwekeza na  kufanya biashara ili kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.  

Aidha, Dkt. Kijaji amesema Serikali inaendelea kufanya mamoresho mbalimbali kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini ( Blueprint) ikiwemo kupitia na kurekebisha sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Uwekezaji pamoja na  kupunguza tozo mbalimba ambazo zimekuwa kikwazo katika ufanyaji biashara na uwekwzaji.

Naye Mkurugenzi huyo wa Kikanda chini ya Benki ya Dunia amesema Programu hiyo ya kukuza  uchumi  na Taasisi amesema Benki dunia kupiyia programu hiyo iko tayali kuwawezesha wajasilimali watanzania katika sekta mbalimbali kuendeleza biashara zao zitakazoongeza ajira, pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi kwa ujumla.