Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

Suma JKT watakiwa kuharakisha ujenzi wa jengo la utawala la Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO


Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) kwa niaba ya Waziri Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameitaka Suma JKT kuharakisha ujenzi na uboreshaji wa jengo la utawala la TIRDO kwa mujibu wa mkataba wa kazi hiyo.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo Machi 17, 2023 katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la TIRDO ambalo halijakamilika kulingana na mkataba.

Wakichangia Kwa nyakati tofauti mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la TIRDO, Maabara ya Nishati na Kitengo Cha teknolojia, Waheshimiwa wajumbe wa Kamati hiyo wameonesha kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na TIRDO Katika kuwasaidia hasa vijana kufanya na kuendeleza bunifu zao.

Vilevile Waheshimiwa wajumbe wa kamati hiyo wamesema  kuwa wanafahamu umuhimu wa TIRDO kwa maendeleo ya viwanda hapa nchini hivyo watahakikisha wanalisimamia Shirika hilo pamoja na kukuza bunifu zilizopo ambazo zinahitajika katika kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii.