Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

Wanawake na Vijana ni Injini ya Biashara Afrika 


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema ni muhimu kuwawezesha wanawake na vijana katika biashara ili waweze kutumia fursa zilizopo katika  Eneo huru la Biashara Barani Afrika AfCFTA .

Amesema kuwa,Tanzania na Bara la Afrika wakiwekeza zaidi katika sayansi na teknolojia kwa vijana wanaweza kuwa sehemu muhimu ya kustawisha uchumi kama ilivyo kwa Taifa la China.

Dkt  Kijaji ameyasema hayo alipokuwa akimkaribisha Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Samia Suluhu Hassan  wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya AFCFTA Septemba 12, 2022 jijini Dar es salaam .

"Ni imani yetu kwamba, wote tutatumia nafasi hii vizuri, kwa kuibua mijadala mipana itakayoleta tija kwa maendeleo ya Afrika yetu, hasa tukilenga kuwajengea uwezo wa kibiashara wanawake na vijana kwa kutoa mapendekezo ambayo yatazingatiwa katika maandalizi ya Itifaki ya wanawake na vijana katika biashara ambayo inalenga la kutatua changamoto za ushiriki wa wanawake na vijana katika biashara barani Afrika na hata dunia kwa ukubwa wake,"amesema Waziri Dkt.Kijaji.

Awali Mheshimiwa Waziri Dkt.Kijaji amesema,mkutano huo utajadili mada mbalimbali muhimu ikiwemo changamoto wanazokumbana nazo Wanawake na Vijana katika biashara za Mpakani (Reflecting on Challenges Women and Youth face in Cross Border Trade in Africa).

Pili ni namna ya kusaidia wanawake na vijana ambao ni kichocheo katika Sekta ya Ubunifu Barani Afrika (Supporting Women and Youth as Drivers of the Creative Industry in Africa);

Mada ya tatu ni juu ya namna ya kutumia nyenzo za kidigitali za biashara ili kuimarisha ushindani wanawake na vijana katika Soko la Eneo Huru la Afrika la Biashara (Leveraging Digital Solutions to Trade to Enhance Women’s and Youth’s Competitiveness in the AfCFTA Market).

Nne, ni namna ya kusaidia urasimishaji wa biashara za wanawake na wijana ili waweze kunufaika zaidi na Mkataba wa Eneo Huru (Women and Youth in Informal Cross Border Trade: Supporting the formalization of women and youth in trade for greater benefits under the AfCFTA).

Tano, ni majadiliano kuhusu Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (Youth Roundtable on the AfCFTA Protocol on Women and Youth in Trade).

Sambamba na kuimarisha ushirikishwaji wa Wanawake na Vijana katika masuala ya kifedha (Promoting Financial Inclusion for Women and Youth in Trade).