Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI DKT. KIJAJI ARIPOTI WIZARA NA KUKADHIWA OFISI RASMI.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb) ameripoti Ofisini kwake Mji wa Serikali Mtumba  Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino na kukabidhiwa Ofisi kutoka kwa Waziri mstaafu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo

Dkt. Kijaji amepokelewa na Naibu waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe aliyeambata na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godius Kahyarara na watumishi wa wizara hiyo. 


Aidha, Dkt. Kijaji amepata fursa ya kukutana na Menejimenti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kusisitiza kila mmoja kufanya kazi kwa bidii "sisi ni moyo wa uchimi wa Taifa letu, tukifanya vema Taifa letu litaendelea kuwa na uchumi imara zaidi.


Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ni Wizara yenye Muundo mpya kufuatia mabadiliko ya muundo wa Wizara na uteuzi wa Mawaziri , Naibu Mawaziri, Katibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu uliofanywa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 08 Januari 2022