Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Viwanda na Biashara
Mwisho: 14th Sep 2020
Request for Consultancy To Review and Develop National Policy and Legal Framewor...
Mwisho: 28th Apr 2020
Request for Expression of Interest Title: Consultancy to Develop a National Dat...
Imewekwa: 01st February, 2021
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini. Akizungumza na wazalishaji hao kutoka Kiwanda cha sukari Mtibwa, Kilombero, Kagera,TPC, Manyara, Bodi ya Sukari pamoja na Chama cha wazalishaji sukari nchini (TPSA) leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kutatua changamoto walizonazo ili kuongeza uzalishaji wenye tija kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji. ”Leo nimekutana na nyie kwa lengo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi ili tuongenze uzalishaji utakaokidhi mahitaji ya sukari nchini”amesema Mhe.Mwambe. Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili kuongeza uzalishaji wa sukari utakaokidhi mahitaji ya sukari nchini bila kuagiza sukari kutoka nje na ziada iuzwe nje ya nchi. Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.