Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. Innocent Lugha Bashungwa (MP)

Wasifu

Ziara ya Naibu waziri kiwanda cha Mazava Mkoani Morogoro


Imewekwa: 20th August, 2018

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) atembelea kiwanda cha Mazava kilichopo mkoani Morogoro. Katika ziara hiyo Naibu Waziri amepokea taarifa ya kiwanda ambacho kinaendelea na uzalishaji wa fulana na bukta mbalimbali ambazo kwa asilimia 100 husafilishwa nje ya nchi kwa mauzo, Kiwanda kimeajiri wafanyakazi 2180 wenye mikataba ya kudumu ambao asilimia 70 ni wanawake na asilimia 30 ni wanaume pia kiwanda kinaendesha programu ya mafunzo kwa Vijana 210 ambao huajiriwa na kiwanda baada ya kuhitimu kuziba nafasi mbalimbali kiwandani hapo. Meneja Msaidizi wa kiwanda cha Mazava, ndugu Nelson Mathias Mchuke alimweleza Naibu Waziri changamoto mbalimbali za kiwanda ikiwemo ufinyu wa eneo la uzalishaji kwani kiwanda kimekodi eneo jingine lakini changamoto imekuwa ni idhini ya kutumia eneo husika, pia ubovu wa Barabara kufika na kutoka kiwandani hapo. Meneja Msaidizi wa Kiwanda hicho amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi anazofanya kupitia Viongozi aliowateua kwani serikali ya awamu ya tano imeweza kutatua changamoto mbalimbali kiwandani hapo ikiwemo ya umeme. Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya, amewapongeza menejimenti ya kiwanda kwa kutengeneza ajira kubwa katika Mkoa wa Morogoro, pia amewahakikishia kushughulikia changamoto walizomweleza kwa haraka zaidi hasa ya kuanza kutumia jengo jipya ambalo litaongeza ajira ya watu 1000.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2020. Haki zote zimehifadhiwa.