Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Majukumu ya Wizara

Wizara ya Viwanda na Biashara ina dhamana ya kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera na mikakati inayosimamia maendeleo ya viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo. Majukumu mahsusi ya kisekta ni pamoja na:-

  1. Kuandaa, kuratibu na kupitia sera na mikakati ya sekta za viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo;
  2. Kufuatilia na kufanya tathmini (M&E) ya utendaji katika viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo na Taasisi zinazowezesha maendeleo ya viwanda na biashara;
  3. Kuimarisha ufanisi wa utendaji wa wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zake;
  4. Kukusanya, kuchambua, kusambaza na kutathmini taarifa za sekta za viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo;
  5. Kutafuta fursa za masoko ya bidhaa za Tanzania ndani na nje;
  6. Kubuni na kuandaa programu za kuendeleza sekta za viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo na Taasisi zinazowezesha maendeleo ya viwanda na biashara;
  7. Kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Sekta Binafsi;
  8. Kukuza na kuhamasisha biashara ya ndani na nje na kuboresha upatikanaji wa huduma za kuendeleza biashara;
  9. Kusimamia utekelezaji wa sheria zinazosimamia viwanda, biashara masoko na Viwanda vidogo Vidogo;na
  10. Kuimarisha utafiti wa maendeleo ya Sekta ya Viwanda na Biashara;