UWEKEZAJI

UWEKEZAJI

Tanzania ni eneo la kimkakati kijiografia na lenye rasilimali nyingi zenye kuvutia uwekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi zikiwemo viwanda, madini, utalii, kilimo na biashara. Uwekezaji huo ambao hufanywa kwa kiwango kikubwa na Sekta Binafsi umechochewa na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na mfumo wa kitaasisi na kisheria wa kusimamia uwekezaji nchini. Mifumo hiyo, pamoja na mambo mengine, inatoa...

Majukumu

Kuandaa na kusimamia  utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na Miongozo ya uwekezaji nchini

Kuhamasisha na kutoa ushauri kuhusu uwekezaji katika sekta zote

Kutoa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji nchini kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi

Kuwezesha uwekezaji kutoka nje katika sekta zote za uchumi

Kusimamia utendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania

Sera & Mikakati

Sehemu ya Uendelezaji wa Uwekezaji

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
 • Sehemu ya Uendelezaji wa Uwekezaji inatekeleza majukumu yafutayo:-

  • Kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuwezesha uwekezaji wa ndani na nje;
  • Kuratibu na kufuatilia vikao vya Ndani na Kimataifa ili kuboresha mahusiano   na mazingira ya uwekezaji;
  • Kuwezesha uingiliaji  wa Taasisi kwa wakati husika ili kutatua vikwazo vinavyowakabili wawekezaji;
  • Kuwezesha majadiliano na usimamizi wa mikataba katika miradi ya kimkakati ya uwekezaji wa ndani na nje; na
  • Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Kitaifa ya   Uendeshaji Uwekezaji (NISC

  Sehemu ya Ufuatiliaji

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
 • Sehemu ya Ufuatiliaji inatekeleza Majukumu yafuatayo:-

  • Kuandaa, kupitia na Kusimamia utekelezaji wa sera ya Uwekezaji, sheria, kanuni, miongozo, mikakati, mipango na programu;
  • Kuandaa na kutekeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya uwekezaji;
  • Kufuatilia na kutathmini utekelezaji  wa mikataba  ya miradi ya uwekezaji;
  • Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa miradi ya uwekezaji inayofanywa na Wakala wa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine;
  • Kufanya utafiti wa mara kwa mara kuhusu masuala yanayohusu uwekezaji wa nje na ndani katika sekta zote; na
  • Kutathmini athari za uwekezaji kijamii kwa kuzingatia sera ya uwekezaji

  Sheria ya Uwekezaji, 2022

 • star
 • star
 • star
 • star
 • star
 • Sheria ya Uwekezaji, 2022

  Taasisi zilizo chini ya Wizara

  Wasiliana Nasi

  • Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
  • Mji wa Serikali, Mtumba, Mtaa wa Viwanda S.L.P 2996, 40478, Dodoma Jengo la Mambo ya Nje 4th Floor Shaaban Robert Street, Dar es Salaam, Tanzania
  • 0
  • 0
  • info@mit.go.tz