Wizara ya Viwanda na Biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara

Hon. Innocent Lugha Bashungwa (MP)

Wasifu

UJUMBE WA UKARIBISHO TOKA KWA WAZIRI

Uongozi na Menejimenti nzima pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wanapenda kuwakaribisha wadau wote kwenye Tovuti ya Wizara. Tovuti hii imesanifiwa kiufundi na maalum kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wadau ndani na nje ya nchi juu ya masuala ya Sekta ya Viwanda, Biashara, Masoko, Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo.

Tovuti hii imesanifiwa kutoa fursa za kipekee ambazo zinawaunganisha wadau kwenye sekta ambazo zinahusiana. Wadau watanufaika kwenye mambo yahusuyo Sera, Mikakati, Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ambazo zinaonesha jitihada katika mtangamano wa Viwanda, Biashara, Masoko pamoja na huduma mbalimbali zinazoiunganisha Tanzania na Dunia.

Wananchi pia watajulishwa juu ya hatua za maendeleo ambazo Tanzania imefikia katika mashirikiano ya kiuchumi na mtangamano wa kibiashara. Pia, wajasiriamali wataunganishwa na taasisi za fedha na huduma zingine za muhimu kwa maendeleo ya ujasiriamali ikiwemo fursa za mikopo yenye masharti nafuu, elimu ya biashara, maarifa na kuibua fursa za maendeleo.

Wadau wataunganishwa na fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zipo kwenye sera na mikakati mbalimbali iliyopo ambazo pia zinawaunganisha na Sekta binafsi chini ya ubia wa sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Pamoja na hayo, wataunganishwa na taasisi za kisekta na zingine katika kuendeleza Viwanda, Biashara, Masoko, Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo na Uwekrzaji.

Ni tumaini langu kuwa wadau wote wa ndani na nje ya Tanzania ambao wana matarajio na dhamira nzuri ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi wataitumia ipasavyo na hivyo, kunufaika kutokana na mwongozo na fursa mbalimbali zilizopo kwenye Tovuti ili kuwanufaisha na kuchangia kwa mtu mmojammoja na jumuiya yote duniani.

Wizara iko tayari kupokea maoni ili kuboresha Tovuti ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa. Tovuti itaendelea kuwa haina hivyo kwa muda wote itaendelea kuboresha utoaji wa huduma zake ikitambua Mpango Mkakati, Mkataba wa Huduma kwa Mteja pamoja na kuzingatia miongozo ya kushughulikia malalamiko. Milango itabaki kuwa wazi na tunaomba ushirikiano wenu wa dhati.

PAMOJA TUNAWEZA.

Hatimiliki © wizara ya viwanda na biashara 2020. Haki zote zimehifadhiwa.