ARCHIVES

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na SIDO imeandaa na  kutoa mafunzo kwa wajasiriamali 108 kutoka kanda tatu kwa kuanzia. Kanda hizo ni Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Manyara na Singida), Kanda ya Pwani (mikoa ya Morogoro, Dar es salaam na Pwani), Kanda ya Kaskazini (mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro).

 

Madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwaongozea ujuzi na kuwapa uelewa zaidi wajasiriamali kuhusu taratibu muhimu katika kufanikisha uzalishaji bidhaa bora na taratibu zinazochangia kwa wajasiriamali kuweza kumudu ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

 

Mafunzo haya yametolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo wa nchi za Ulaya katika mradi  wa EDF-10 unaotekelezwa na Wizara ya Viwanda na Biashara. Aidha, Wizara itaendelea kutoa mafunzo (mafunzo endelevu) kama haya kwa wajasiriamali wengi zaidi nchini kulingana na upatikanaji wa fedha.

 

Elimu iliyotolewa kwa wajasiriamali ni pamoja na masuala ya  sheria zinazohusu uasilia wa bidhaa (rules of origin), ufungashaji bora, ufuatiliaji wa bidhaa ilikotengenezwa (traceability), utambuzi wa bidhaa, mapatano na mikataba ya biashara.

 

Mafunzo hayo yalifanyika kutoka tarehe 09/05/2012 hadi 12/05/2012 katika vituo vitatu vya Singida, Moshi na Kibaha na yaliendeshwa na wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania Bureau of Standards (TBS), Small Industries Development Organization (SIDO) na GS1 (T) National Ltd wakisaidiana na maafisa kutoka wizarani.

 

Mafunzo hayo yalilenga kuwaelimisha wajasiriamali wadogo juu ya

  • Mfumo wa ufuatiliaji (traceability) wa bidhaa ilikotengenezwa
  • Umuhimu na matumizi ya alama za utambuzi (Barcodes) katika bidhaa na kupata uelewa juu ya kampuni ya GS1 (T) NATIONAL LIMITED inayoshughulikia masuala ya alama za utambuzi (Barcodes).
  •  Ufungashaji bora wa bidhaa wanazotengeneza.
  • Uwekaji wa alama na lebo katika bidhaa wanazozalisha.  
  • Sheria za uasilia(rules of origin) na kukuza uelewa wa wajasiriamali kuhusu chama cha wafanya biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) wenye mamlaka ya kutoa cheti cha uasili “Certificate of Origin”, inayowawezesha wajasiriamali kuuza bidhaa zao katika soko la Afrika Mashariki, SADC na AGOA kwa unafuu zaidi.
  • Mbinu za kufanya mapatano ya kibiashara na mambo ya kuzingatia katika kusaini mikataba itakayoleta tija kwao.

 

Utaratibu wa kutoa mafunzo kama hayo ni moja ya mikakati iliyowekwa na Wizara ya kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuboresha bidhaa wanazozalisha. kwa kutambua mchango wa sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo katika kukuza uchumi wa taifa. 

 

 

Bwana Henrick Mdede, Mwezeshaji toka SIDO makao makuu akitoa mafunzo kuhusu kanuni za uasili, kwa wajasiliamali toka mikoa ya Singida, Manyara na Tabora, mjini Singida katika ukumbi wa Social Training Centre tarehe 11/05/2012.

 


Wajasiriamali wanaosindika mafuta ya alizeti  kutoka Singida , Manyara na Tabora wakijadili matatizo yanoyoikabili sekta ya usindikaji alizeti.Wajasiriamali kutoka katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam, wakipata mafunzo mjini kibaha.Wajasiriamali katika kituo cha Singida wakifuatilia kwa makini somo la ufungashaji lililoendeshwa na Bwana Hamisi Sudi Mwanasala,  Afisa Viwango Mwandamizi toka TBS,  hayuko pichani.Wajasiriamali wa mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro, wakijadili  katika makundi mjini Moshi.Washiriki kwenye kituo cha Singida katika picha ya pamoja baada ya kufunga mafunzo hayo tarehe 12/05/2012. Aliyekaa katikati ni Mgeni rasmi Bwana  Francis Mashuda, Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Singida , na kushoto kwake ni Bi Fransisca Masawe, Meneja wa SIDO mkoa wa Singida.Aliyekaa kulia kwake ni Bwana Nyango  Mbogora, Afisa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara Idara ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo.Aliyesimama wa kwanza kulia ni Bwana Hamisi Sudi,  mtaalamu toka TBS.Mkurugenzi wa idara ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Bwana Burhani Mlundi (aliyevalia suti nyeusi katikati,mstari wa mbele wliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali na wawezeshaji katika kituo cha Kibaha siku ya kufunga mafunzo tarehe 12/5/2012


Message from the PS

blockquote

This website is posted for the purposes of providing Stakeholders with the necessary information on role and functions of MIT. It covers the key sectors of Industry, Trade & Marketing.

To facilitate the development of sustainable industry and trade sectors through creation of enabling environment and provision of improved services.


 

By Permanent Secretary - MIT

Contacts

 

address

Address
Ministry of Industy & Trade 
NSSF Waterfront,1st Floor,
35 Edward Sokoine Road, 11469

Dar es Salaam

 
phone

Telephone:
+255-22-2127898/97

 
email

email:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

hit counters